Cars and buses driving on city road

Kazi zetu

Kazi kubwa ya TADIO ni kusimamia maslahi ya redio stesheni zinazofika vijijini pamoja na wasikilizaji wake waliopo maeneo hayo kupitia ushawishi wa kuundwa sera bora za kurusha matangazo, mafunzo na kutengeza mtandao kati ya vituo vya redio na kutoa nafasi/fursa kwa washirika wetu kuwafikia zaidi wasikilizaji waliopo vijijini. TADIO iko katika maandalizi ya kuanzisha redio mtandaoni itakayoitwa Redio TADIO ambayo itatumika kutoa habari mubashara kabisa kwa watu waliopo vijijini na mjini.

Cars and buses driving on city road

Kazi ya uchechemuzi

TADIO inafanya kazi kubwa kwa niaba ya redio jamii zilizopo nchini, kushawishi na kushauri Serikali pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania

Lengo kuu ni  kulinda maslahi ya redio hizi na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa.

Kuwajengea uwezo

TADIO pamoja na washirika wetu huandaa mafunzo na kuwaalika watangazaji na wazalishaji wa vipindi kutoka redio wanachama wetu. Hii ni kwa lengo la kutengeneza ushirikiano baina ya redio wanachama wetu nchini Tanzania.

Lengo ni kuboresha uhusiano  baina ya redio wanachama wetu nchini Tanzania.

Hivi karibuni redio wanachama wetu walipewa mafunzo juu ya utangazaji wa taarifa kuhusu maswala ya uchaguzi, jinsia, mazingira na maswala ya biashara na kupewa mafunzo ya tehama. Wengine walipewa mafunzo juu ya maswala uongozi ya kwa ujumla. Kuanzia Mwaka 2020 tumejikita zaidi kwenye vitendo ili tuweze kuzoea mfumo wetu mpya wa kurusha matangazo kwa njia ya mtandao.

Jinsi ya kuwafikia watu waishio vijijini

Idadi kubwa ya watanzania wanaishi vijijini. Zipo asasi nyingi zisizo za serikali, taasisi za serikali, mashirika ya misaada na mashirika na biashara ambao wangependa kufikia watu waishio vijijini kwa lengo la kuwaelimisha kuhusu maswala ya kijamii, afya, kufanya kampeni na pia kutangaza masoko au kutangaza huduma fulani kwa watumiaji waliopo maeneo ya vijijini.

TADIO ni msaada mkubwa kwa  mashirika na makampuni haya katika kuwafikia watu waishio vijijini kwa kutumia mtandao wa redio zake. Hili linaweza kufanyika kupitia kutengeneza ushirika wa pamoja kupitia kudhamini matangazo au vipindi vya redio. Hii itasaidia  kuvipatia vituo vyetu vya redio kipato kwa ajili ya kujiendesha.

Redio jamii ya mtandao

Redio ya mtandaoni iitwayo Redio TADIO imeanza mwaka huu 2020. Kituo hicho kipya ni kwa ajili ya kutoa taarifa na kurusha matangazo ya redio jamii  kupitia  matukio yanayokea vijijini katika jukwaa la kitaifa.

Redio TADIO itakuwa na kazi ya kuchapisha habari, kupiga picha, habari sauti na kurusha taarifa mubashara kupitia mtandao. Lengo la jukwaa hilo ni kuwa sehemu ambayo inatembelewa na watu wengi ili kujua na kufahamu mada mbalimbali kuhusu watu na mambo ya maeneo ya vijijini, “Kwa uhakika wa habari za vijijini” kama inavyonukuliwa na  Mwenyekiti wa TADIO Bwana Baptist John Mutesasira.